Klabu ya Azam FC imetangaza rasmi kutumia Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kwa ajili ya michezo yake ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Uamuzi huo unaifanya Azam FC kuungana na watani wao wa soka, Yanga SC, ambao pia watatumia uwanja huo kwa ajili ya michezo yao ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
Kwa upande mwingine, klabu ya Simba SC itatumia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchezwa kwa michezo yake ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hatua hiyo inaifanya Zanzibar kuwa moja ya vituo muhimu vya soka la kimataifa kwa Tanzania, huku timu tatu kubwa zikiwakilisha nchi katika mashindano ya klabu barani Afrika.