Simba SC vs Mashujaa FC, Uwanja wa Uhuru

MCHEZO mkali wa NBC Premier League unatarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Uhuru, Simba SC vs Mashujaa FC.

Simba SC ni vinara wenye pointi 21 baada ya mechi 7 wanawakaribisha Mashujaa FC walio nafasi ya 4 kwenye msimamo wamevuna pointi 12 baada ya mechi 7.

Pambano hili la kukata na shoka linatarajiwa kupigwa saa 1:00 usiku. Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita Simba SC ilitoka kuvuna pointi 3 kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga SC.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Simba SC amesema wapo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.

“Tumetoka kucheza mchezo mgumu dhidi ya Yanga SC na kupata pointi 3 hivyo tunakwenda kwenye mchezo mwingine ambao tunaamini utakuwa na ushindani mkubwa,”.

Steven Ndorobo, Ofisa Habari wa Mashujaa FC amesema wamefanya maandalizi mazuri wataingia kwa tahadhari kusaka pointi 3 muhimu.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar

Moyo Wangu Unavuja Damu: https://selar.com/7901h4koj4