UONGOZI wa Fountain Gate umebainisha kwamba upo tayari kuwakabili wapinzani wao JKT Tanzania katika mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa leo Oktoba 9,2026.
Pambano hili la NBC Premier League linatarajiwa kupigwa saa 8:00 mchana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika msako wa pointi 3 muhimu kwa kila timu.
Kwenye msimamo Fountain Gate ipo nafasi ya 15 ina pointi 4 inakutana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 11 na pointi 7 zote zimecheza mechi 6.
Issa Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate amesema wanatambua ushindani ni mkubwa na kila timu imejipanga kusaka ushindi wapo tayari kupambania matokeo mazuri.