SIMBA SC maandalizi yamepamba moto kuelekea mechi za msimu wa 2026/27 ambazo zina ushindani mkubwa kwa kila timu.
Kikosi cha Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker kimeweka kambi nchini Afrika Kusini ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi hayo.
Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kambi hiyo ya siku 10 gharama zote zimefanywa na Mo ambaye ni Rais na Mwekezaji wa Simba SC.
“Kambi yetu ya Afrika Kusini ni maalumu kwa ajili ya mechi zilizopo kwenye mashindano kitaifa na kimataifa. Kwa wachezaji ambao hawapo kwenye timu za taifa walipewa mapumziko na yalipoisha wakarejea kambini,”.
Mchezo ujao wa Simba SC ni Oktoba 10, 2026 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo.