Timu ya Taifa ya Sudan U-20 imeandika historia baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya CECAFA U-20 kwa mara ya kwanza, ikiifunga Tanzania kwa mikwaju ya penalti 4-3, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1 katika fainali iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Ushindi huo umeipa Sudan taji lake la kwanza katika historia ya mashindano hayo, baada ya kufika fainali kwa kuifunga Uganda mabao 3-2 katika hatua ya nusu fainali. Sudan ililazimika kupambana kutoka nyuma kabla ya kupata ushindi huo muhimu.
Kwa upande wa Sudan, mafanikio hayo yanaongeza uzito wa kampeni yao katika mashindano haya, kwani timu hiyo pia imefanikiwa kufuzu kwa AFCON U-20 2027 nchini Ghana.
Sudan na Tanzania ndizo timu mbili kutoka ukanda wa CECAFA zilizopata nafasi ya kushiriki michuano hiyo ya fainali .