Simba SC yapiga kambi Afrika Kusini siku 10

MSAFARA wa kikosi cha Simba SC, mapema Septemba 24, 2026 umekwekea pipa kuelekea  Afrika Kusini kwa maandalizi ya mechi za kitaifa na kimataifa.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker kituo kinachofuata kwenye ligi ni dhidi ya Yanga SC, mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2026.

Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kambi hyo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mechi zilizopo mbele yao kitaifa na kimataifa.

“Rais wa Simba SC na mwekezaji, Mohammed Dewji tunamshukuru kwa kujitoa kwake kugharamia kambi hii ya siku 10. Hii ni maalumu kujifua katika eneo lenye utulivu na kuwafanya wachezaji kuwa na deni kwa mechi zinazofuata,”.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni David Kameta, Kibabage, Hamza Jr, Hussen Abel. Nyota Neo Maema, Rushine hawa wapo Afrika Kusini wataungana na timu kambini.

Ligi imesimama kwa muda kutokana na uwepo wa mechi za kuwania kufuzu AFCON 2027 na Tanzania ni miongoni mwa timu ambazo zitakuwa na kazi kusaka ushindi licha ya kufuzu kwa kuwa watakuwa wenyeji.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar