Mkude alimpiga mkwara kocha

LEGEND ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Jonas Mkude kiungo wa Mashujaa FC ameweka wazi kuwa alipokuwa ndani ya Yanga SC alimpa kazi ngumu Kocha Mkuu Miguel Gamondi kwa wakati huo kuhusu uwezo wake kwenye mechi za kimataifa.

Mkude amebainisha kuwa kuna siku Gamondi alimuuliza kama anaweza kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika jambo ambalo aliona analimudu.

“Mwalimu aliniuliza unaweza kucheza mchezo huu wa kimataifa? Kwa kuwa aliniuliza basi nikaona hapa nimpe maelezo kwanza aone kama ninaweza ama sitaweza.

“Unajua ilibidi iwe hivyo kwa sababu kwanza anaona sijapata nafasi yakucheza muda mrefu na siku hiyo kwenye hiyo nafasi hakuna mtu mwingine.

“Nikamwambia nina uzoefu wakucheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali mechi 8 nje na ndani, uliza hapa kwenye kikosi nani ana rekodi hii?

Rekodi hiyo Mkude aliandika akiwa anacheza katika kikosi cha Simba SC. Katika maisha ya soka Mkude amecheza timu 3 kubwa ndani ya ligi mpaka sasa alianza na Simba SC, Yanga SC na sasa Mashujaa FC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar