
Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili kipa wa Aston Villa na Argentina, Emi Martínez, kwa ada ya takribani Sh bilioni 26.98.
Chelsea imekuwa ikihitaji kipa mpya kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, huku Martínez akitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho huo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Martínez atasaini mkataba wa miaka miwili, ukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa sehemu muhimu ya Aston Villa tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2020, akicheza zaidi ya mechi 250.
Martínez pia ni mmoja wa makipa waliotajwa kuwa bora duniani, huku akiwa na mchango mkubwa katika kuisaidia Argentina kutwaa Kombe la Dunia 2022, ikiwemo kuokoa mpira muhimu katika dakika za mwisho za fainali dhidi ya Ufaransa.
Uhamisho huo ukikamilika, Martínez atakuwa akielekea Stamford Bridge kuimarisha safu ya magolikipa ya Chelsea.
