Azam FC 2-0 Tanzania Prisons, hali ni tete

Azam FC 2-0 Tanzania Prisons, hali ni tete kwa wajelajela kutokana na mwendo usiofurahisha ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC Premier League.

Baada ya dakika 90, Mei 22, 2026 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 2-0 Tanzania Prisons, magoli ya Feisal Salum dakika ya 15 na Idd Nado dakika ya 62.

Ushindi huo unawapa pointi 3 muhimu Azam FC wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 49 baada ya mechi 24 ndani ya msimu wa 2025/26.

Tanzania Prisons hali inakuwa tete kwa kuwa wanapambana kujinasua kutoka mstari wa kushuka daraja jambo linalowapa ugumu kwenye mechi zilizobaki kupata pointi 3.

Baada ya mechi 24 wapo nafasi ya 15 wakiwa na pointi 17, timu inayoshika mkia ni KMC FC ambayo ina pointi 10 hizi zote zipo kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja hali ikiwa ni tete.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.