Allen Okello anakera kinomanoma

Allen Okello kiungo mshambuliaji wa Yanga SC anakera kinomanoma kama hayupo upande wako kutokana na kujiamulia mambo kwenye mechi ngumu NBC Premier League.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Mei 22, 2026 dhidi ya Singida Black Stars alijiamulia kufunga magoli mawili wakishinda magoli 3-0.

Okello alifungua ukurasa wa magoli dakika ya 14 na 68 na goli la moja lilifungwa na kiungo Mudathir Yahya dakika ya 41 pointi tatu zikibaki Jangwani.

Timu hiyo inafikisha jumla ya pointi 57 ndani ya ligi ni vinara wakiwa tofauti ya pointi 2 na mtani Simba SC mwenye pointi 55 nafasi ya pili kwenye msimamo.

Wababe hawa wote wawili wamecheza jumla ya mechi 24, mchezo ujao kwa Yanga SC ni Mei 25, 2026 itakuwa dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa KMC Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.