Meridianbet Yaendeleza Upendo kwa Jamii Kupitia Msaada kwa Watoto wa Magomeni

Katika kuendeleza moyo wa kusaidia jamii, Meridianbet imetoa msaada wa vyakula kwa kituo cha watoto cha UMRA Children Center kilichopo Magomeni, Dar es Salaam kama sehemu ya shughuli zake za kijamii.

Msaada huo umehusisha bidhaa muhimu za chakula kama mchele, unga, sukari, mafuta ya kupikia pamoja na mahitaji mengine yanayotumika kila siku katika kituo hicho cha watoto.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Akizungumza mbele ya viongozi wa kituo hicho, Nancy Ingram kutoka Meridianbet alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali zinazosaidia watoto na makundi mengine yenye uhitaji maalum nchini.

“Jamii yenye furaha hujengwa kwa kusaidiana. Tunafurahi kuona msaada huu ukienda kuwasaidia watoto hawa na kuleta tabasamu katika maisha yao ya kila siku,” alisema mwakilishi huyo.

Uongozi wa UMRA Children Center umeeleza kuwa msaada huo ni faraja kubwa kwa watoto wanaolelewa hapo na umeishukuru Meridianbet kwa kuendelea kuonyesha moyo wa kujali jamii ya Watanzania.