Manchester United wanaripotiwa kuwa na nia ya kumsajili kiungo wa kati wa West Ham, Mateus Fernandes, kwa mujibu wa The Telegraph.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kuondoka West Ham katika dirisha lijalo la majira ya joto, hasa kutokana na hali ya klabu hiyo inayokabiliwa na hatari ya kushuka daraja. West Ham kwa sasa wameingia tena kwenye eneo la kushuka daraja na wako nyuma kwa pointi moja dhidi ya Tottenham huku zikiwa zimesalia mechi tatu kabla ya msimu kumalizika.
Fernandes ameonyesha kiwango kizuri katika msimu wake wa kwanza akiwa West Ham baada ya kujiunga akitokea Southampton, ambao nao walishuka daraja msimu uliopita. Uhamisho wake uliripotiwa kugharimu takribani pauni milioni 38, na ameendelea kuwa mchezaji muhimu katikati ya uwanja.