Vita ya Ya EPL Aston Villa Kuishusha Daraja Tottenham leo? Soma zaidi Uchambuzi

Mechi ya leo Uwanja wa Villa Park inakutanisha timu zinazopambana kwa malengo tofauti kabisa, huku Aston Villa wakiwa katika nafasi ya 5 kwenye msimamo wakipambana kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na Tottenham wakiwa mateso katika nafasi ya 18.

Villa wakiwa na pointi za kutosha kujiweka kwenye nafasi ya kuwania miamba ya Ulaya, huku Tottenham ikiwa nyuma kwa pointi mbili kukwepa daraja na michezo minne tu imesalia. Timu zote mbili zina njaa ya ushindi lakini kwa sababu tofauti Villa wanataka kusherehekea msimu mzuri nyumbani, huku Spurs wakipambana kwa uhai wao wa Ligi Kuu.

Kocha wa Aston Villa Unai Emery anaweza kutumia safu ya inayomtegemea Ollie Watkins mbele, huku kocha wa Tottenham Roberto De Zerbi akijaribu kukabiliana na msururu wa majeruhi wanaomkosesha wachezaji wake wakuu. De Zerbi ana presha kubwa la kuhakikisha timu yake haishuki daraja katika klabu kubwa kama Tottenham.

Tottenham wamekumbwa na majeruhi wengi sana, wakiwemo Xavi Simons aliyethibitishwa kuwa na jeraha na Dominic Solanke mfungaji wao mkuu anayekosa mechi kwa jeraha la paja . Kwa upande wa Aston Villa, watawakosa nyota wake Amadou Onana anayekosa kwa jeraha la magoti, hivyo wanaweza kumtegemea Ollie Watkins anayechanganya ulinzi kwa kasi yake pamoja na Emiliano Martinez mabingwa wa dunia langoni.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Villa wamekuwa wakiwachapa Tottenham kwenye michezo ya karibuni, wakiwa na ushindi wa mwendelezo wa 4 kwenye michezo ya Ligi Kuu kati yao ikiwemo ushindi wa 2-1 ugenini mnamo Oktoba 2025 na 2-0 nyumbani Mei 2025.

Tottenham wana historia ndefu ya kuwaongoza Villa kwa ushindi zaidi (19 dhidi ya 9) lakini mwendelezo wa hivi karibuni unaonyesha Villa wamekuwa wao ndio watawala . Katika michezo 8 ya karibuni kati ya timu hizi, michezo 5 imekuwa na mabao 2 au 3 huku mabao yakifungwa pande zote mbili kwa urahisi. Jisajili

Tottenham wakiwa na njaa ya kuokoa daraja, wanaweza kusukuma mbele na kufunga pia kwa kutumia kasi ya wachezaji kama Mathys Tel na Richarlison, hivyo tunaweza kuona mechi ya mabao mengi na burudani ya dakika zote 90.