Yanga SC vs Tanzania Prisons kupigwa KMC Complex

YANGA SC vs Tanzania Prisons NBC Premier League ni leo Aprili 4, 2026 Uwanja wa KMC Complex saa12:30 jioni.

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema kuwa ataendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji ambao hawapo fiti lakini wapo tayari kwa ajili ya kupambania pointi tatu.

“Tumekuwa na mazoezi mazuri ya kujiandaa dhidi ya Tanzania Prisons, akili zetu zinawaza kufanya vizuri tu. Tunajua nini tunataka, ni wazi tunacheza na timu ngumu, tunakumbuka ugumu tuliopata katika kushinda mechi ya mzunguko wa kwanza. Licha ya hali hiyo, lakini tupo hapa kwaajili ya alama tatu na tuna imani tutazipata.

“Bado tunachangamoto kubwa ya majeruhi ya wachezaji wetu muhimu, mfano Job, Mzize na wengine, lakini timu nzima ina lengo la kupata matokeo mazuri. Hivyo kila mtu anafanya jitihada kubwa kutimiza malengo ya klabu.

“Tunawashukuru sana Wananchi kwa kuwa nasi katika kila hali, hasa baada ya ratiba yetu ngumu. Licha ya kuwa na matokeo ya kusuasua katika mechi kadhaa zilizopita, lakini mashabiki wetu hawajawahi kuwa nyuma, wanakuja kutupa sapoti.

“Licha ya majeruhi tulionao, tuna wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa sana lakini wanaopaswa kuanza ni 11 pekee. Nafurahi kuwa wachezaji wote wana uelewa mkubwa kuhusu mawazo yetu na mbinu tunazowapa. Naamini kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kuisaidia timu, naamini itakuwa siku ngumu lakini nzuri kwasababu tumekuja kusaka ushindi,”.

Yanga SC kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 38 inakutana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 13.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.