MCHEZO wa NBC Premier League umekamilika kwa wababe wawili kutoshana nguvu baada ya dakika 90.
Ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid umesoma TRA United 0-0 Yaga SC wakigawana pointi mojamoja.
Kiungo mkabaji wa TRA United, Mzamiru Yassin alionyeshwa kadi mbili za njano hali iliyopelekea kuonyeshwa kadi nyekudu dakika ya 85.
Matokeo hayo yanafanya Yanga SC kufikisha mchezo wa 15 bila kufungwa ndani ya ligi msimu wa 2025/26 wakifikisha jumla ya pointi 37 wanaongoza ligi.
TRA United inafikisha pointi 20 inasalia nafasi ya 10 baada yakucheza jumla ya mechi 15 ndani ya ligi.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.