Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amempongeza kiungo wa klabu hiyo, Bruno Fernandes, baada ya mchezaji huyo wa Ureno kutoa asisti mbili kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Everton siku ya Jumapili.
Nahodha huyo wa Man United amefikisha jumla ya asisti 16 kwenye Ligi ya Uingereza msimu huu, akivunja rekodi ya David Beckham ya asisti 15 kama mchezaji mwenye asisti nyingi zaidi kwa msimu mmoja wa Ligi Kuu England katika historia ya klabu.
Mreno huyo sasa anaangalia kufikia au kuvunja rekodi ya asisti nyingi zaidi kwenye msimu mmoja wa Ligi Kuu England inayoshikiliwa na Thierry Henry na Kevin De Bruyne, kila mmoja akiwa na asisti 20.
Kwa jumla, Bruno Fernandes amefikisha mchango wa magoli 205 kama mchezaji wa Manchester United kwenye michuano yote, akiwa amefunga magoli 105 na kutoa asisti 100 katika mechi 319 za klabu hiyo.
Akizungumza kupitia BBC Radio 5, Rooney alisema:
“Bruno ndiye aliyeleta utafauti katika ushindi huu muhimu kwa Man United. Kwa mtazamo wangu, ndiye mchezaji bora msimu huu wa Ligi Kuu England.”
Je, unakubaliana na Rooney kwamba Bruno Fernandes ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu England msimu huu?