Taarifa zinadai kuwa Shirikisho la Soka la Angola (FAF) lipo kwenye mazungumzo na kocha Florent Ibenge (64) ili kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Angola.
Ibenge anatajwa kuchukua nafasi ya Patrice Beaumelle (47), kocha raia wa Ufaransa ambaye hivi karibuni aliondoka kwa makubaliano ya pande zote na shirikisho hilo na kwenda zake KUJIUNGA na kikosi cha Esperance de Tunis.
Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo yapo na ni mazuri mno, huku mjadala mkubwa ukihusu masuala binafsi ikiwemo mshahara ili kuhakikisha saini ya Ibenge inapatikana.
Je, tajiri na mmiliki wa Azam FC, Yusuf Bakhresa atakubali kuona Florent Ibenge anaiacha Azam FC na kwenda kuitumikia timu ya taifa ya Angola? Hilo ndo la kujiuliza..