Aziz Ki Amzawadia Hamisa Gari ya G-Wagon ya Milioni 300

Kiungo nyota wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki, ambaye hivi karibuni ameondoka Wydad Athletic Club na kujiunga na Al Ittihad Club ya Libya, amemzawadia mke wake, Hamisa Mobetto, gari la kifahari aina ya Mercedes Benz G-Class (G-Wagon) lenye thamani zaidi ya TSh milioni 300.

Zawadi hiyo imekuja ikiwa ni maadhimisho ya mwaka mmoja wa ndoa yao

Aziz Ki aliposti video kupitia Instagram yake akiambatanisha na ujumbe wa kugusa hisia akisema:

“One year today. Thank you God.
I’m grateful for the peace, the growth, and the prayers we share.
This is just a small gesture to say thank you for being the woman you are, patient, strong, loving, and full of light.
No amount of gifts, no expensive gift I am going to give you that would say how much I love, cherish, and adore you, my beautiful wife. You are a blessing in so many ways.
May GOD continue to guide us, protect our home, and increase us in love and understanding, now and forever. 🤍
Nakupenda Sana @hamisamobetto 🌹❤️”

Hamisa Ajibu kwa Shukrani

Kwa upande wake, Hamisa aliandika kwa hisia akisema:

“God really said ‘now watch what I do for her.’
Ahsante Mungu wangu kwa kunionekania 🥺💕🙏🏽”

Mashabiki mitandaoni wamepongeza zawadi hiyo wakieleza kuwa ni ishara ya mapenzi, heshima na kuthaminiana ndani ya ndoa yao.