Wilfred Ndidi Aahidi Kulipa Bonus Zote Za Wachezaji wa Nigeria Kabla ya Mchezo wa Robo Fainali

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Nigeria, Wilfred Ndidi, amewaahidi wachezaji wenzake na benchi la ufundi kuwa atahakikisha bonus zote wanazodai kutoka uongozi wa juu zinatolewa kabla ya mchezo muhimu wa Robo Fainali dhidi ya Algeria utakaopigwa Jumamosi.

Ndidi amewauliza wachezaji wenzake kuendelea na mazoezi ya maandalizi bila hofu yoyote, akisisitiza kwamba ikiwa bonus hizo hazitapatiwa kufikia siku ya Jumamosi, atazilipa yeye binafsi.

Nigeria tayari wamesafiri kuelekea Marrakech, Morocco, kwa ajili ya mchezo huo wa Robo Fainali, huku mshambuliaji Victor Osimhen akiwa sehemu ya kikosi hicho.

Hii ni hatua inayojiri huku Nigeria ikiweka mikakati ya kuhakikisha wanashiriki kwa ubora mkubwa na kuongeza nafasi ya kufika hatua ya nusu fainali katika mashindano ya kimataifa.