Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza hafla ya kuwapongeza wanamichezo wa Tanzania waliofanya vizuri na kulitangaza Taifa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, hii leo Januari 10, 2026, Ikulu Dar es Salaam wakiongozwa na wachezaji wa Timu ya Taifa Stars waliofanikiwa kufika hatua ya 16 bora katika mashindano ya AFCON-2025 yaliyofanyika nchini Morocco.
Rais Samia Awapongeza Wachezaji wa Taifa Stars Baada ya AFCON-2025 – Video