Morocco 2-0 Comoros ni matokeo ya mchezo wa ufunguzi AFCON 2025, nchini Morocco huku wenyeji wakipata ushindi katika kipindi cha pili.
Magoli ya Morocco yamefungwa na Brahim Diaz kwa pasi ya N.Mazraoui dakika ya 55 na El Kaabi kwa pasi ya Salah-Eddine dakika ya 74, mchezo uliochezwa Uwanja wa Prince Moulay Abdallah.
Ikumbukwe kwamba Brahim Diaz ambaye ni mfungaji wa goli la kwanza ni kinara wa utupiaji katika mchakato wa kufuzu AFCON 2025. Alifunga jumla ya magoli 7 kwenye nyavu ameanza kazi yake aipendayo.
Wenyeji Morocco wameanza kampeni kusaka taji la AFCON 2025 kwa ushindi mchezo wa ufunguzi. Kwenye mchezo huo Morocco walikuwa na nafasi ya kupata goli la kuongoza dakika ya 11 kupitia mkwaju wa penalti ambao walipata. Shukrani kwa mlinda mlango wa Comoros Yannick Pandor ambaye aliokoa pigo la penalti iliyopigwa na Soufiane Rahims.
Gumzo limekuwa ni goli la pili kwa Morocco ambalo lilifungwa kipindi cha pili. Mtupiaji Ayoub El Kaabi alifunga goli hilo kwa mtindo wa acrobatics. Goli hilo linatajwa kuwa katika orodha ya magoli ambayo yatawania tuzo ya goli bora katika mashindano ya Afcon 2025.
Chini ya Kocha Mkuu, Walid Regragui Morocco wamezianza vema kampeni kwa ushindi kwenye mchezo wa kundi A. Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kuongoza kundi ikiwa na pointi 3.
Group A
1. Morocco pointi 3 wamecheza mchezo nmoja
2. Mali pointi 0 hawajacheza mchezo hata mmoja
3. Zambia pointi 0 hawajacheza mchezo hata mmoja
4. Comoros pointi 0 wamecheza mchezo mmoja.
Ratiba ya AFCON 2025
Leo Jumatatu, Desemba 21,2025
Mali vs Zambia
Afrika Kusini vs Angola
Misri vs Zimbabwe
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.