Yanga SC yataja siku ya beki wa kazi kurejea uwanjani

UONGOZI wa Yanga SC umebainisha kuwa nyota wa kikosi hicho ambaye hakuwa kwenye mechi za ushindani kwa muda mrefu anatarajiwa kurejea uwanjani rasmi 2026.

Ni beki wa kupanda na kushuka Yao ambaye hajaonekana uwanjani msimu mzima wa 2024/25 na 2025/26 kwenye mechi za awali hakuwa katika mipango ya benchi la ufundi zaidi ya kuendelea na matibabu.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema kuwa wachezaji ambao walikuwa na majeraha habari njema ni kwamba wanazidi kuimarika kutokana na matibabu ambayo wamepata.

“Tuna wachezaji ambao walipata majeraha na kuna wachezaji ambao hawakuonekana kwenye mchezo wetu dhidi ya Coastal Union. Kutoka kwenye idara yetu ya madaktari nianze kwa kutoa ripoti ya wachezaji ambao wapo kwenye matibabu na mchezaji wa kwanza ni Kouassi Yao ambaye ni habari njema kwa mashabiki wa Klabu yetu.

Yao ameshamaliza kipindi chake cha kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na sasa yupo chini ya uangalizi wa fitness na hiyo ni hatua kubwa sana kwa Yao kurejea tena Uwanjani, na anatarajiwa kuwa tayari kati ya mwezi januari mwishoni au februari mwanzoni,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.