Yanga SC vs Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuchezwa Oktoba 28,2025 Uwanja wa KMC Complex.
Huo ni mchezo wa ligi ambapo Yanga SC imetoka kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Silver Striker katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kuelekea mchezo huo mchezaji Clement Mzize ambaye ni mshambuliaji atakosekana kwa kuwa hayupo fiti asilimia 100 baada ya kujitonesha eneo la goti alipokuwa mazoezini.
Yanga SC ni mabingwa watetezi wa ligi mchezo wao uliopita kwenye ligi walitoshana nguvu na Mbeya City kwa kugawana pointi mojamoja.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi katika mchezo huo muhimu.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.