MSHAMBULIAJI wa Yanga, Prince Dube gari limewaka wanasema kutokana na kasi yake kuzidi kuimarika kwenye kucheka na nyavu kwenye mechi za ushindani ndani ya uwanja.
Bado ana deni la kuongeza mwendo ili kufunga mabao mengi kwa kuwa kwenye mechi za hivi karibuni amekuwa akikosa umakini kwenye nafasi anazopata kamailivyokuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar licha ya kutoa pasi moja ya bao.
Kwenye ligi namba nne kwa ubora Dube alianza kwa kusuasua ambapo alifungua akaunti yake ya mabao kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex ilikuwa ni Desemba 19 2024 alipofunga mabao matatu.
Dube aliandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya ligi inayodhaminiwa na NBC kufunga hat trick akisepa na mpira wake na alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo.
Kwenye mchezo wa CRDB Federation dhidi ya Copco alifunga bao moja kati ya matano akitumia pasi ya beki Israel Mwenda.
Rekodi zinaonyesha kuwa Dube amecheza mechi 14 za ligi akifunga mabao matano na kutoa pasi tatu za mabao hivyo kahusika kwenye mabao 8 kati ya 36 yaliyofungwa na Yanga iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake kibindoni 42.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.