MASTAA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids wanatarajiwa kuukosa mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos, kutokana na sababu za kiufundi.
Ikumbukwe kwamba katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa wa hatua ya makundi ulipowakutanisha Simba na Bravos, pointi tatu zilibaki Dar.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-0 Bravos kwa bao la Jean Ahoua ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti bao hilo lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Ni Joshua Mutale, Steven Mukwala, Aishi Manula, Duchu, Nouma hawa hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kimataifa ugenini dhidi ya Bravos, Januari 12 2025 kwenye msako wa pointi tatu.
Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa watawakosa wachezaji hao kutokana na sababu za kiufundi.
“Kuna wachezaji ambao tutawakosa kwenye mchezo wetu dhidi ya Bravos ikiwa ni Manula, Mukwala, Duchu hawa wote inatokana na sababu za kiufundi hivyo benchi la ufundi limeamua iwe hivyo na sisi tunawaheshimu wapinzani wetu.
“Unaona Balua hakuwa kwenye mechi kwa muda lakini amerejea ikiwa ni tayari kwa ajili ya mechi zetu zijazo, kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mechi yetu na ile ya mwisho Uwanja wa Mkapa itakuwa ni kazi kwa mashabiki kuujaza uwanja.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.