SIMBA QUEENS WAITULIZA YANGA PRINCESS
KWENYE ulimwengu wa soka la Wanawake Tanzania ushindani unazidi kuwa mkubwa kila iitwapo leo ambapo mchezo mkali wa Kariakoo Dabi uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ni Simba Queens waliibuka wababe. Baada ya dakika 90 kwenye mchezo huo ubao ulisoma Yanga Princess 0-1 Simba Queens huku bao la ushindi likifungwa na Vivian Corazone kipindi cha pili….