KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema kuwa watafanyia kazi makosa yaliyotokea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Ramovic kukaa benchi baada ya kurithi mikoba ya Miguel Gamondi alishuhudia ubao ukisoma Yanga 0-2 Yanga na mabao yote yakifungwa kipindi cha pili.
Unakuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Yanga kupoteza ndani ya msimu wa 2024/25 ambapo ni mechi mbili zilikuwa za ligi zama za Gamondi na moja kwenye anga la kimataifa.
Kocha huyo amesema walijitajihidi wachezaji kutafuta matokeo lakini walikwama kutokana na kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kwenye mchezo huo.
“Wachezaji walijitahidi kutafuta matokeo lakini haikuwa hivyo na unajua kwamba bado hatujawa na muda mrefu ya maandalizi ya pamoja kutokana na hali ilivyo bado wachezaji hawajawa fiti tunaamini tutafanyia kazi makosa ili kuwa bora wakati ujao.”
Ni dakika 270, Yanga safu yake ya ushambuliaji imefunga bao moja ilikuwa dhidi ya Tabora United kwenye mechi tatu mfululizo mtupiaji alikuwa ni Clement Mzize ambaye hakuwa fiti baada ya kupata maumivu akiwa kwenye majukumu ya taifa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.