KITAWAKA LEO MASHUJAA FC DHIDI YA ‘WANA LUNYASI’, SIMBA SC KATIKA DIMBA LA LAKE TANGANYIKA, KIGOMA

Ligi Kuu ya soka ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo Novemba Mosi, 2024 kwa mchezo mmoja ambapo kutakuwa na pambano la kukata na shoka kati ya Wazee wa ‘Mapigo na Mwendo’, Mashujaa Fc dhidi ya ‘Wana Lunyasi’, Simba Sc katika dimba la Lake Tanganyika, Kigoma.

Mchezo huo utakaopigwa mishale ya saa 10:00 jioni ni wa nne baina ya timu hizo kwenye michuano yote huku Mnyama akishinda mara mbili, kipigo kimoja na sare moja.

Ushindi utawapeleka Simba Sc mpaka nafasi ya pili wakifikisha pointi 22 wakiwa sawa na Singida Black Stars lakini Wekundu hao wa Msimbazi watabebwa na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mashujaa Fc vs Simba Sc
Lake Tanganyika
Saa 10:00 jioni