WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa Rais wa Marekani uliopangwa kufanyika
Novemba 5, 2024 likipanda, kampuni nyota ya michezo ya kubashiri nchini, LEONBET
imetangaza kuwapa fedha watakaobashiri kiusahihi matokeo ya wagombea, Donald Trump na
Kamala Harris.
Meneja Mkuu wa LEONBET Tanzania, Tumaini Maligana amesema kuwa wameamua kupanua
wigo wa kubashiri kwa wafuatiliaji wa siasa ili na wao waweze kufaidika kupitia ubashiri wao.
Maligana amesema kuwa hii ni nafasi yao ya kipekee ya kutumia maarifa yako kushinda pesa
kupitia uchaguzi wa Marekani ambao unatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwa wagombea hao
wawili.
“Cha kuvutia zaidi, sasa unaweza kubeti matokeo haya kupitia LEONBET, kampuni mpya ya
kubashiri nchini Tanzania iliyokuja na nguvu kubwa, odds za kibabe, na malipo fasta,” amesema
Maligana.
Kwa mujibu wa Maligana, kwa zaidi ya miaka 15 katika sekta ya kubashiri, LEONBET
imefanikiwa kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wateja wake ulimwenguni kote.
“Sasa, kampuni hii yenye uzoefu mkubwa imekuja Tanzania na inaleta mabadiliko makubwa
kwenye soko la kubeti mtandaoni.
Kwa watumiaji wa Tanzania, LEONBET inaleta mambo mengi ya kuvutia kama Odds Kubwa –
Beti zako zinaweza kukupatia ushindi mkubwa zaidi na pili malipo ya haraka ambayo
uwawezesha washindi kupata malipo papo hapo,” amesema.
Pia amesema kuwa kampuni yao imepanua wigo wa kubashiri (Masoko Mengi ya KubetI) ambayo
inawapa fursa wapenda michezo, siasa, au burudani na vile vile kuwapa nafasi ya FREEBET
hadi kufikia Sh8, 000 kwa wateja wapya.
“Unapojisajili leo, unapewa FREEBET hadi Sh8, 000 kwenye mwezi wako wa kwanza. Hii ni
nafasi yako ya kuanza bila ya kuwekeza pesa zako mwenyewe na kuongeza nafasi yako ya
kushinda.” Alisisitiza.
Alisema kuwa ili kuwapa wateja wao huduma bora zaidi, wameamua kuwa hewani kwa wateja
wao kwa masaa 24 katika wiki (24/7) na kuwa na michezo ya mingi mbalimbali.
“Kwa wateja wa LEONBET, huduma ya wateja inapatikana masaa 24 siku saba (7) wiki ili
kuhakikisha unapata msaada unaohitaji kila wakati. Unaweza pia kufurahia michezo mingi ya
kubashiri – iwe ni mpira wa miguu, michezo ya kasino, au matukio makubwa kama uchaguzi wa
Marekani,” amesema Maligana.