HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA NA MATOKEO

BAADA ya Coastal Union ya Tanga kushuhudia ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ukisoma Coastal Union 0-1 Yanga, Oktoba 26 2024 kuna kibarua kingine kinafuata leo.

Oktoba 29 Coastal Union itawakaribisha Kagera Sugar mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 10:15 jioni.

Ken Gold mapema saa 8:00 mchana watakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Dodoma Jiji hii ni Oktoba 29.

Oktoba 30 ni Singida Black Stars dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa saa 2:30 usiku itakuwa Zanzibar.

Oktoba 28 2024 matokeo Bongo ilikuwa hivi:-

Fountain Gate 2-2 Mashujaa, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mabao ya Seif Karihe dakika ya 15 na Hassan Ali dakika ya 28 kwa Mashujaa na yale ya Fountain Gate mtupiaji ni Nicholas Gyan dakika ya 34 na Salum Kihimbwa dakika ya 90.

Namungo FC 1-0 Pamba Jiji bao la Namungo limefungwa na Ibrahim Ali Mkoko dakika ya 14 Uwanja wa Majaliwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.