CLEMENT Mzize mshambuliaji wa Yanga ana maajabu yake ndani ya Bongo kutokana na kupenya katika kikosi cha kwanza mbele ya miamba Prince Dube, Jean Baleke, Kennedy Musonda ambao wote ni washambuliaji akiwa na kazi kubwa ya kufanya kutimiza majukumu yake.
Ipo wazi kwamba kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Mzize alianzia benchi na alipopata nafasi ya kuingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Dube aliandika bao lake la kwanza ndani ya ligi msimu wa 2024/25.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga bao la kwanza lilifungwa na Maxi Nzengeli ambaye ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao manne ndani ya ligi kwenye kikosi cha Yanga.
Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Mzize alianza kikosi cha kwanza na benchi kulikuwa na Baleke.
Ana kazi kubwa ya kufanya kuboresha makosa kwenye mechi anazocheza ili kuwa bora zaidi ikumbukwe kwamba alipata nafasi ya kucheza Kariakoo Dabi Oktoba 19 2024.
Mbele ya Ken Gold alikomba dakika 67 alipoanza kikosi cha kwanza ambapo kilipata ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Sokoine bao la ushindi lilifungwa na Bacca akitumia pasi ya kiungo mshambuliaji Aziz Ki.