MSANII WA VICHEKESHO WA KITAMBO, PEMBE AMEFARIKI DUNIA

Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, Pembe amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.

Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Dar, Francisco Mwinuka almaarufu Pierre, amethibitisha na kueleza kuwa kwa sasa anaelekea Hospitali ya Temeke na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.