>

AZAM FC YAVUNJA BENCHI ZIMA LA UFUNDI

RASMI ungozi wa Azam FC umefikia makubaliano ya kuvunja benchi la ufundi lililokuwa chini ya Kocha Mkuu, Yusuph Dabo raia wa Senegal.

Taarifa iliyotolewa na Azam FC mapema Septemba 3 2024 imeeleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC na kocha Youssouph Dabo wamefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea kufanya kazi pamoja kuanzia Septemba 3 2024.

Dabo aliyehudumu Azam FC kwa kipindi cha mwaka mmoja anaondoka na wasaidizi wake wa benchi la ufundi aliokuja nao.

Klabu pamoja na wadau wake inapenda kumshukuru Dabo kwa weledi wake na moyo wake wa kutokata tamaa katika kipindi chote alichokuwa na timu ns kumtakia kila la kheri huko aendako.

Aidha wakati bodi ikiwa kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya, programu za timu zitakuwa chini ya makocha wa timu za vijana.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa mwisho kwa Dabo kukaa kwenye benchi la ufundi ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania ambao ulikuwa wa ligi wakitoshana nguvu kwa kugawana pointi mojamoja.