MICHAEL Fred mshambuliaji wa zamani wa Simba amesema kuwa ikiwa atakuwa ndani ya Ligi Kuu Bara ana amini kwamba ikiwa atakuwa ndani ya Ligi Kuu Bara atakuwa mfungaji bora kwani kutokana na uwezo wakufanya hivyo ndani ya uwanja.
Msimu wa 2024/25 Fred akiwa na uzi wa Simba alifunga jumla ya mabao sita na miongoni mwa timu ambazo alizifunga ni Yanga kwenye Kariakoo Dabi mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ukasoma Yanga 2-1 Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Fred amesema kuwa anatambua uwezo alionao kwenye kufunga mabao ndani ya uwanja hivyo yeye ni mfungaji bora na ikiwa atakuwa ndani ya Bongo atakuwa bora.
“Nipo Tanzania kwa sasa ninaheshimu nafasi ambayo nilipewa ndani ya Simba kwa kuwa ni timu bora maisha yalikuwa mazuri kikubwa ni kuona maisha yanaendelea. Ikiwa nitakuwa ndani ya ligi ya Tanzania nina amini kwamba nitakuwa mfungaji bora kwa kuwa nina uwezo huo.
“Ligi imekuwa na ushindani mkubwa na wachezaji wanajituma ndani ya uwanja hilo lipo wazi kwa kuwa msimu unaanza tunaamini kuna mengi ambayo yatatokea ndani ya uwanja.”.
Inaelezwa kuwa nyota huyo yupo kwenye hesabu za timu za Bongo ambazo zinahitaji kupata saini yake mshambuliaji huyo maarufu kwa jina la fungafunga.