>

TATU ZAIPA BAO SIMBA NA TATU ZAIPONZA

MWENDO wa pasi tatu ilikuwa Uwanja wa KMC, Complex kwa Simba na Al Hilal kufunga bao mojamoja katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ambapo ni pasi tatu ziliipa bao la kuongoza na pasi tatu zikaiponza Simba kwenye eneo la ulinzi ndani ya dakika 90.

Ni Simba walianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 25 ilikuwa ni pasi kuanzia kwa Mavambo kisha Ladack Chasambi akatoa pasi ya bao kwa Leonel Ateba ilikuwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Nyota huyo Ateba alifunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Simba msimu wa 2024/25 kipindi cha kwanza akiwa ndani ya uwanja Agosti 31 2024.

Bao la Al Hilal pia ilikuwa pasi tatu zilipigwa baada ya Simba kupoteza mpira ndani ya 18 eneo la Al Hilal ilikuwa dakika ya 75 na bao likafungwa na Serge Pokou.

Hivyo kila timu ililipa kisasi kwa mpinzani wake kwa mwendo uleule hivyo kuna kazi kubwa kwa timu hizo kufanyia maboresho hasa eneo la ulinzi na ushambuliaji kwenye kumalizia nafasi ambazo zinatengenezwa ndani ya uwanja.