KAGERA SUGAR KUWAKARIBISHA YANGA KAITABA

MABINGWA mara 30 ndani ya Ligi Kuu Bara Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi leo Agosti 29 2024 itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar.

Kagera Sugar wanawakaribisha mabingwa watetezi waliotwaa taji msimu wa 2023/24 na baada ya kucheza mechi 30 ni pointi 80 walikomba jumlajumla.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-0 Yanga.

Gamondi amesema matokeo yaliyopita wanasahau kwa kuwa ni msimu mpya na mashabiki wanahitahi pointi tatu kwenye mchezo huo.

“Matokeo ambayo yamepita hayo nimewaambia wachezaji wasahau kikubwa ni kuona kwamba kwenye mchezo wetu tunafanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu.”

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliopo kwenye kikosi hicho ni Aziz Ki, Pacome, Kibabage, Bakari Nondo ambaye ni nahodha.

Dickson Job beki wa Yanga msimu wa 2023/24 ni yeye alikuwa mfungaji wa bao la kwanza ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.