MASTAA sita wa Simba inayoongoza Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 wameitwa kwenye majukumu yao ya timu ya taifa kwa ajili ya kuwania kufuzu AFCON 2025.
Ipo wazi kwamba Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwenye mechi mbili za ligi ambazo ni dakika 180 imekomba jumla ya pointi sita na safu ya ushambuliaji imefunga mabao saba kinara wa utupiaji akiwa ni Valentino Mashaka mwenye mabao mawili.
Wachezaji watatu ambao wameitwa nje ya Bongo ni Valentin Nouma Burkina Faso,
Steven Mukwala staraika refu kuliko goli Uganda na Moussa Camara huyu ni mlinda mlango waGhana.
Kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni mastaa watatu pia wameitwa ikiwa ni Ally Salim huyu ni mlinda mlango, Mohamed Hussen beki wa kupanda na kushuka, Edwin Balua kiungo mshambuliaji.