MATAJIRI wa Dar, Azam FC chini ya Kocha Mkuu Yusuph Dabo wanafungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya JKT Tanzania.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Azam FC iligotea nafasi ya pili na kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo imegotea hatua ya awali.
APR ya Rwanda imewafungashia virago Azam FC kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 kwa sababu mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, ilikuwa Azam FC 1-0 APR ule wa pili uliochezwa Rwanda ilikuwa APR 2-0 Azam FC.
Mchezo wa ufunguzi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Meja Isamuhyo, Jumatano saa 10.00 jioni kwa kila timu kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.
Azam FC ina mastaa ikiwa ni kiungo mshambuliaji Feisal Salum ambaye msimu wa 2023/24 alikuwa kwenye ubora wake alipofunga jumla ya mabao 19 kinara wa utupiaji akiwa ni Aziz Ki wa Yanga ambaye alitupia mabao 21.