SALEH JEMBE: SIMBA HAIMHITAJI MANULA, BUSARA ZITUMIKE KUMALIZANA – VIDEO

Mchambuzi mahiri wa soka, Saleh Ally Jembe @salehjembefacts amesema mashabiki wa Simba waliomzomea mchezaji wao, Kibu Denis kwenye mechi dhidi ya APR ya Rwanda kwenye Simba Day, walikuwa sahihi kutokana na utovu wa nidhamu waliofanyiwa na mchezaji huyo.

Saleh amesema Kibu Denis pia hakupaswa kucheza kwenye mechi hiyo kwani hakushiriki kwenye mazoezi ya pre-season kama wenzake kutokana na sakata lililokuwa likiendelea kati yake na uongozi wa Simba.