MBAYA WA SIMBA ATUA YANGA

MABOSI wa Yanga wamekamilisha dili la kuinasa saini ya mshambuliaji mwenye kupenda kufunga akiwa ndani ya uwanja jambo ambalo linaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya mabingwa wa ligi Yanga msimu wa 2023/24.

Nyota huyo alikuwa akiwapa tabu makipa wengi Bongo ikiwa ni pamoja na wale wa Simba ikiwa ni pamoja na Aishi Manula, Ayoub Lakred, Ally Salim walipokuwa wakikutana kwenye mashindano mbalimbali,

Ikumbukwe kwamba matajiri wa Dar, Azam FC walieleza kuwa walipokea ofa kutoka kwa Simba ikihitaji huduma ya Dube wakati mchezaji huyo alipoomba kuvunja mkataba wake.

Dube alivunja mkataba na Azam FC kwa kufuata masharti yaliyokuwa kwenye mkataba wake hivyo alikuwa huru kujiunga na mabingwa wa msimu wa 2023/24 Yanga.

Raia huyo wa Zimbabwe amesaini dili la miaka miwili kuitumikia timu ya Yanga atakutana na Simba ndani ya ligi kwenye Kariakoo Dabi akiwa na uzi wa Yanga.

Msimu wa 2023/24 walipokutana na Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na bao la Simba lilifungwa na Clatous Chama ambaye kwa sasa yupo ndani ya Yanga.