>

AUSTRIA YAMALIZA KILELENI KUNDI D, UFARANSA NAFASI YA PILI

Timu ya taifa ya Ufaransa imelazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Poland katika mchezo wa raundi ya tatu wa Kundi D kwenye EURO 2024. Sare hiyo inaifanya Ufaransa kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo ingawa tayari ilishafuzu hatua ya mtoano.

Katika mchezo mwingine wa kundi D, Austria imebainisha Uholanzi 3-2 na kumaliza kileleni mwa Kundi hilo huku ikifuzu hatua ya 16 bora.

FT: Ufaransa 🇫🇷 1-1 🇵🇱 Poland
⚽ Mbappé 56’
⚽ Lewandowski 79’

FT: Uholanzi 🇳🇱 2-3 🇦🇹 Austria
⚽ Gakpo 47’
⚽ Depay 75’
⚽ Malen (og) 6’
⚽ Schmid 56’
⚽ Sabitzer 80’