RAIS WA YANGA AMPOKEA MGENI WAKE ACHRAF KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA KILIMANJARO

Rais wa klabu ya @yangasc Mhandisi Hersi Said @caamil_88 amempokea Mgeni wake Achraf Hakimi @achrafhakimi katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Mchezaji huyo kutoka katika Klabu ya Paris Saint German (PSG) ya nchini Ufaransa ameambatana na rafiki zake saba atakuwa nchini kwa wiki moja huku wakitembelea vivutio mbali mbali vya utalii nchini.