CHAMA NA SIMBA NGOMA NZITO ISHU YA KUONGEZA MKATABA MPYA

NGOMA ni nzito kwa mabosi wa Simba dhidi ya kiungo mshambuliaji Clatous Chama kuhusu ishu ya kuongeza mkataba mpya ndani ya kikosi hicho.

Kiungo huyo msimu wa 2023/24 alotupia mabao saba na pasi sita za mabao mkataba wake umegota mwisho na hajaongeza dili jipya kutokana na kinachoelezwa kuwa anahitaji mshahara wa zaidi ya milioni 30.

Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa mchezaji huyo mkataba wake umeisha na kinachofanyika kwa sasa ni mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba mpya ama kumuacha yote kwa maslahi ya Simba.

“Mchezaji Clatous Chama mkataba wake umeisha hivyo suala lake linafanyiwa kazi viongozi wanazungumza ili kutambua itakuaje hivyo nikipata taarifa juu yake nitaweka wazi.

“Kama itakuwa ni kuongeza mkataba ni kwa maslahi ya Simba na kama itakuwa ni kuamua kumuacha itakuwa ni kwa maslahi ya Simba pia, mashine ya kuongelea, semaji la CAF bado sijapata taarifa kutoka kwa uongozi. “