MERIDIANBET YATOA MSAADA KWA WAKAZI WA KIBAHA

Kwa mara nyingine Meridianbet wamefanikiwa kufika wilaya ya Kibaha na kutoa msaada katika eneo hilo katika makundi mbalimbali ya kijamii.

Wababe hao wa michezo ya kubashiri wameendelea kuhakikisha wanarudisha kwa jamii yao inayowazunguka, Ambapo wamefanikiwa kuwagusa makundi mawili ya kijamii ambapo wametoa msaada familia duni pamoja watu wenye ulemavu wa ngozi (Ualbino)

Mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wamefanikiwa kutoa mafuta (Lotion) maalumu ambayo hutumika na watu wenye Ualbino ili kuzuia ngozi zao kupigwa na jua lakini pia zinaacha ngozi ikiwa katika muonekano mzuri, Meridianbet pia walihakikisha wanatoa msaada wa mahitaji ya nyumbani katika familia duni zinazopatikana eneo hilo.

Suka mkeka wako kwenye michuano ya Euro 2024 inayoendelea nchini Ujerumani sasa ujishindie Mamilioni. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Kaimu wa kitengo cha Mawasiliano na masoko kutoka kampuni ya Meridianbet bwana Abubakar Kulindwa alipata nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya taasisi na kusema “Nina furaha kubwa kuwepo mahala hapo leo kutimiza hili ambalo tumelifanya leo la kurudisha kwenye jamii yetu kidogo tulichonacho, Lakini pia nipende kutoa shukrani kwa ukaribisho mzuri tuliopata kutoka kwa wakazi wa Kibaha”

Wakazi wa eneo hilo nao walipata nafasi ya kuzungumza ambapo wameonesha kutoa shukrani zao kwa kampuni ya Meridianbet kwa kuwakumbuka na kutoa witu kwa makampuni mengine kuiga mfano kwa mabingwa hao wa michezo ya kubashiri.