USAJILI WA YANGA BALAA ZITO LINAKUJA

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa utafanya usajili wa kishindo katika dirisha kubwa la usajili ambalo limefunguliwa Juni 15 2024.  Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi ina mpago wa kuongeza washambuliaji pamoja na mabeki katika kikosi kwa msimu ujao.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24 wataipeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Wataungana na Azam FC, matajiri wa Dar.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua kazi kubwa inapaswa kufanyika ili kupata kikosi bora zaidi jambo ambalo linafanyiwa kazi.

“Tutafanya usajili wa kishindo tunatambua kwamba ili kuwa bora ni muhimu kuwa na kikosi imara jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa umakini mkubwa.

“Kila kitu kipo kwenye mpango kazi na malengo yetu ni kuona kwamba tunakuwa imara kwa ajili ya msimu mpya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tunaamini kwamba kazi itakuwa kubwa.”