KLABU YA PAMBA JIJI FC YATHIBITISHA KUACHANA NA WACHEZAJI WOTE

Klabu ya Pamba Jiji Fc imethibitisha kuachana na wachezaji wote pamoja na benchi lote la ufundi ambao waliipandisha timu daraja kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumalizika kwa mikataba Yao klabuni hapo.
Pamba Jiji FC ambayo imepanda daraja kuja Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu ujao ipo kwenye mchakato wa kutengeneza timu mpya kwaajili ya msimu unaokuja.