LIVE BUNGENI: WAZIRI MWGULU ANAWASILISHA MAKADIRIO NA MATUMIZI YA BAJETI KUU YA SERIKALI 2024/2025


Serikali imesema bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 imelenga kutekeleza vipaumbele vitakavyojikita katika kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu” pamoja na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2024/25.

Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni Dodoma, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameyataja maeneo ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango huo kuwa ni pamoja na kuchochea uchumi shindani na shirikishi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma, kukuza biashara na uwekezaji, kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu.