KOCHA WA VIUNGO AFUNGUKA KUTIMKA YANGA

ALIYEKUWA mtaalamu wa Viungo Yanga, Youssef Ammar amefunguka kuondoka katika klabu hiyo, hivyo hatakuwa sehemu ya Benchi la Ufundi la timu hiyo.
Youssef alisema kuwa anaondoka Yanga, kutokana na shinikizo la Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi, ambaye ameshinikiza kwenda kwa uongozi na kuwaambia anapaswa kuachwa.
Aliongeza kuwa kwa sasa hawezi kuweka wazi kila kitu, lakini yeye hawezi kubembeleza mtu au kumuabudu mtu.