>

RODRYGO ARIPOTIWA KUWAVUTIA MANCHESTER CITY

Rodrygo anaripotiwa kuwavutia Manchester City baada ya kucheza vizuri na kuwa sehemu muhimu katika mafanikio ya Real Madrid msimu huu, akifunga mabao 17 katika michuano yote aliyocheza msimu wa 2023/24 na kutoa pasi tisa za mabao.

City wanathamini uwepo wa Rodrygo katika klabu Madrid, baada ya kumuona kuwa ni mtu anayehitajika kwenye timu lakini Ujio wa Kylian Mbappe unasemekana kutilia shaka kiwango chake msimu ujao.