AZIZ KI BALAA ZITO YANGA

MWAMBA Aziz Ki ana balaa ndani ya uwanja kutokana na kasi yake kuzidi kuwa imara katika uwanja kila wakati.

Rekodi zinaonyesha kuwa amefunga jumla ya mabao 30 ndani ya ligi tangu alipotua Yanga msimu wa 2022/23 na sasa ni 2023/24.

Ni mabao 9 alifunga msimu wake wa kwanza na msimu wa 2023/24 katupia mabao 21 akiwa na tuzo ya ufungaji bora ndani ya ligi licha ya kwamba ni kiungo mshambuliaji.

Kwa msimu wa 2023/24 ni mabao 17 kafunga kwa mguu wa kushoto akiwa ni mkali kwa wenye mabao mengi akitumia mguu huo wa kushoto.

Ipo wazi kwamba Ki ametupia bao moja kwa pigo la kichwa ilikuwa mchezo dhidi ya Tabora United, Uwanja wa Mkapa alipofikisha jumla ya mabao 18 wakati huo kwenye ligi.

Ni Yanga mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24 huku wakiwa na tuzo ya mfungaji bora ambaye ni kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso anatumia jezi namba 10 mgongoni.